Back to Home

1. MAWASILIANO

LUGHA

Lugha ni nini?

Lugha ni mfumo wa sauti za nasibu zenye kubeba maana zilizokubaliwa na jamii ya watu fulani ili zitumike katika mawasiliano.

-      Lugha ndio nyenzo kuu ya mawasiliano baina ya binadamu na binadamu.

-      Kimsingi lugha hutumia sauti zenye maneno ambayo yamepangiliwa kwa njia maalumu ili kuleta maana iliyo kusudiwa.

-      Binadamu hutumia lugha ili kukidhi mahitaji yake ya kila siku, watu hutumia lugha kupashana habari, kubadilisha mawazo.

-      Ili mawasiliano yawepo, mpangilio wa maneno huna budi kuleta maana.

-      Lugha hutofautiana kulingana na watumiaji.

Mfano:

o   Kihaya ni lugha inayotumika na wahaya

o   Kibena ni lugha inayotumika na wabena

o   Kijerumani ni lugha inayotumika na wajerumani

Lugha hujengwa kwa maneno, maneno hujengwa kwa vitamkwa vyenye mpangilio maalum ambao hulipa neno maana. Maneno yakipangwa kwa njia maalum hutoa kauli zenye maana.

Hivyo lugha ili iweze kuleta mawasiliano baina ya wazungumzaji muundo wake huanzia vitamkwa, maneno na hata kauli hupangiliwa kwa njia maalum.

Mfano:

Vitamkwa: - chu, ch, k,a,l,u,o vitamkwa hivi hujenga maneno- chakula, chuo nk.

Katika lugha ya kiswahili vitamkwa hukamilishwa kwa kutumia herufi za alfabeti. Alfabet zimegawanyika katika konsonati na irabu

Konsonati: - b,c,d,f,g,h,j,k,l,m,n,p,q,r,s,t,v,w,x,y,z.

Irabu: -a,e,i,o,u

Kutokana na alfabeti hizi lugha ya kiswahili imejenga maneno mbalimbali ambayo ndio msingi wa mawasiliano kwa watanzania na mataifa mengine.

-      Mawasiliano yasiyotumia sauti sio lugha kwa sababu hapo hutumii sauti wala maneno vilevile mawasiliano ya wanyama, wadudu hayawezi kuitwa lugha kwa sababu hiyohiyo.
 

LUGHA FASAHA

Ni lugha ambayo inafuata taratibu zote za lugha hiyo yaani , kimaana, kimuundo  kimatamshi na kimantiki.

Ili mawasiliano yawe mazuri, wazungumzaji watumie lugha fasaha.
 

(a)  Maana: -

Ili lugha iwe fasaha katika misingi ya maana au msamiati uliokusudiwa, mfano neno barabara lina maana mbili. Mtu anaweza kukosea badala ya kusema njia akasema sawasawa.
 

(b)  Muundo: -

Ufasaha wa lugha hujitokeza kutokana na mpangilio wa maneno kuwa mzuri,

Mfano: - kikubwa kitabu badala ya kitabu kikubwa
 

(c)  Matamshi: -

Sauti za lugha yoyote ile zitamkwe kama zinavyotakiwa ili kujenga ufasaha katika lugha hiyo.

Mfano baadhi ya watu hushidwa kutamka baadhi ya maneno

Mfano: zambi badala ya dhambi

Zarura badala ya dharura
 

(d)  Mantiki

Ili maana iliyolengwa iweze kuwepo kauli lazima ziwe na mantiki

Mfano:  Nimemkuta hayupo badala ya sijamkuta

           Chai imeingia nzi badala ya inzi ameingia kwenye chai
 

ATHARI ZA KUTOTUMIA LUGHA FASAHA

Lugha isipotumika kwa ufasaha

(i) Yaweza kukwamisha mawasiliano

(ii) Lugha hiyo kukosa hadhi na kuonekana kama ya wahuni

Share on WhatsApp Share on Telegram